Helping Hands International kwa kifupi ni (H2i) ni asasi isiyo ya kiserikali
(NGO) ya kimataifa inayojihusisha na kusaidia kundi la watu wenye mahitaji maalum (kama yatima,wajane,
walemavu, waishio katika mazingira magumu)
Mbeba maono wa H2i
ni Mama Luzviminda Mac Elvis, kutoka nchini
ya Ufilipino ambaye baada ya kupitia maisha magumu sana mwanzoni
kutokana na kuzaliwa katika familia duni sana kiasi cha kujikuta anasomeshwa na
mtu kutoka Marekani ambaye hata hakumfahamu kabisa,jambo
lililomfanya aamini kuwa licha ya matatizo anayoweza kukutana nayo
binadamu yeyote akipata mkono wa msaada anaweza kutimiza ndoto
zake.
Imani hii ilimfanya
atafakari sana juu ya watu wenye matatizo kama aliyoyapitia yeye na
ikampelekea kuanzisha mpango wa
kuwasaidia, baada ya yeye kuwa amefanikiwa kutokana na kusaidiwa, akiwa
amehitimu masomo yake na kuajiriwa kwa miaka mingi Marekani alikeleketwa na maono yake ya muda
mrefu aliamua kurejea kwao Ufilipino na kuasisi asasi aliyoiita HELPING
HANDS.
Asasi hii
ilijihusisha na kuwasaidia watoto wa mitaani kurejea shule,kusomesha watoto
yatima, wajane na wanaoishi katika mazingira magumu kuwasaidia kuanzisha miradi
itakayowafanya wajitegemee na kuishi maisha mazuri
Akiwa
anaendelea na kazi zake alikutana na Daktari Ramiel Policarpio,ambaye
alikuwa ni daktari bingwa wa meno huko nchini Ufilipino. Naye alikuwa na
maono yanayokaribiana sana na ya mama Luzviminda. Dr Ramiel alikuwa
inajihusisha na kusaidia ,wazee na wasiojiweza katika nchi hiyo. Walipokutana wakabaini kuwa
maono yao yanafanana na kwamba kwa pamoja wanaguswa na makundi yenye mahitaji
maalumu hivyo waliamua kuunganisha nguvu na kuamua kueneza huduma zao nje ya Ufilipino,yaani
asasi ikawa ya kimataifa, na hapa ndipo jina la asasi hii likabadilika na
kuwa Helping Hands International badala ya *Helping Hands* kama
ilivyokuwa awali. Wakaanza kuenea barani Asia kwa kasi sana kutokana na mguso
wa huduma zao kwa jamii. Jambo hili liliwafanya wakabiliwe na changamoto za
kifedha ili kuwasaidia watu wengi waliojitokeza kutokana na udhamini wa awali
kuzidiwa kabisa. Katika kutafuta suluhu kwa changamoto hii waliamua kubuni na kutafuta vyanzo vya mapato ili kuinua na
kuendeleza huduma hizi.
Kwa
kawaida,Asasi nyingi zisizo za kiserikali (NGO) za kimataifa ama za kitaifa
huendesha shughuli zake za kila siku kwa ufadhili wa makundi mbalimbali kama
vile Serikali , makampuni ya kibiashara ya kimataifa, wafanyabiashara wakubwa
ambao wanatoa misaada kwa jamii ( philanthropists), hivyo basi H2i yenyewe
iliamua kutafuta makampuni makubwa ya kibiashara, ambayo imefanya nayo makubaliano (partnership
agreement) nayo ni kampuni ya magari ya
Hyundai-Korea Kusini, kampuni za computer za HP na Apple za Marekani, na kwa
Nigeria ambako H2i ndio imeanzia kufungua ofisi
katika bara la Africa huko kuna
kampuni kama Diamond Bank,GAC Motors, Glo nk
Pia
,waliamua kubuni chanzo kingine cha mapato ambacho kinatokana na michango
ya wanachama ( Help Partners) ambao wanajiunga kwa hiari yao baada ya kuguswa na matatizo ya watu
waliolengwa na asasi hii na kuamua kuwa sehemu ya utekelezaji wa maono. Hivyo ikapangwa
kuwa mtu yeyote anayetaka kuwa Help partner katika nchi yeyote duniani basi sharti atoe kiingilio cha
(dollar) $40 ( kwa wakati huu ni sawa na
sh 90,000/=) Fedha hii ikitolewa hairudishwi (non refundable). Mchango huu
unatolewa mara moja tu na Help partner na uanachama ni wa kudumu. Pamoja na kuwa kiingilio kinaonekana kidogo lakini
kwa sababu ya uwingi wa Help partners waliopo katika nchi mbalimbali, kiwango hicho kinakuwa kikubwa na hivyo kuweka kufadhili
shughuli za asasi
Ili kuwafikia
walengwa {yatima na wajane} popote duniani
asasi inawatumia Help partners. Help partner ni mtu ambaye ameyaelewa
maono ya asasi na ameaumua kwa hiari yake mwenyewe kuwa sehemu ya kutekeleza
maono hayo yaani kuwafikia na kuyasaidia
hayo makundi husika na ametoa kiingilio na amejiunga kwa kutoa sh 90,000 ( sawa
na $ 40)
JE HELP PARTNER
ANAFAIDIKAJE?
1) Asasi inawatumia Help
partners wake kuwafikia walengwa {makundi ya yatima,wajane }
2)Mpango
wa uwezeshwaji wa H2i. Asasi hii kwa makusudi na kimkakati kabisa imeamua kuwawezesha Help partners wote
kiuchumi
HUDUMA TANO ZINAZOTOLEWA NA
H2i KWA WANACHAMA WAKE [HELP PARTNER]
[Kitendo cha wewe kuamua
kuwa Help partner basi moja kwa moja unanufaika na huduma 5
zifuatazo]
1. HUDUMA YA MISAADA YA KIBINADAMU { HUMANITARIAN SERVICES }
Kuwasaidia yatima,wajane nk- Help partner ndiye anayependekeza yatima, au wajane/kituo cha
yatima, wazee wasiojiweza nk yaani
makundi ambayo yatasaidiwa na H2i (Msaada utatolewa kwa niaba yake
2.HUDUMA YA UWEZESHWAJI WA KIUCHUMI {FINANCIAL EMPOWERMENT
SERVICES}
Mtu
yeyote anapoamua kujiunga na kupata usajili wa kuwa Help partner, anaingizwa
moja kwa moja kwenye mfumo wa kupata fedha
kama bonus mbalimbali kwa kadiri
unavyopanda vyeo katika Asasi hii.[Kuna cheo cha 1 mpaka 6 ] Pia unapata zawadi za vitu vya thamani kama
Laptop, ipad, magari, mkopo wa nyumba, mkopo wa biashara .
Kigezo
cha Help partner kuanza kufaidi huduma hii ni lazima uwashirikishe watu wengine
fursa hii,unatakiwa uwashawishi watu wasiopungua wawili kujiunga na Asasi hii
3. HUDUMA YA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI {TRADE & SKILL
ACQUISITION SERVICES}
Asasi hii
inatambua umuhimu wa kumwendeleza Help partner, kwa hiyo utapata fursa ya
kujifunza ujasiliamali na biashara.
Utafundishwa ujasiriamali wa kutengeneza
vitu mbalimbali kama rangi za nyumba, sabuni nk, pia kujifunza kutunza
kumbukumbu za kifedha
( Utapata
huduma hii utakapokuwa kwenye cheo cha 3).
4. HUDUMA YA MALI NA RASILIMALI {ASSETS
& PROPERTY ACQUISITION SERVICES}
Help
partner anaruhusiwa kukopa au kununua nyumba au kitendea kazi chochote ( Masharti yote ya
ukopaji yatazingatiwa) mkopo hauna riba na unarudishwa ndani ya mwaka mmoja (
Hii inatolewa kwa wale waliofika cheo cha 4 na 5)
5: HUDUMA YA UFADHILI WA MASOMO KWA WATOTO WAKO ( SCHOLARSHIP
AWARD SERVICES)
Kila Help
partner atakeyeingia kwenye cheo cha 5 kwenye Asasi hii atapewa ada ya watoto wake 2, bila kujali kwamba ana watoto au watoto
wake ni wakubwa wanajitegemea au la
H2i INATUMIA MFUMO WA BIASHARA YA MTANDAO {NETWORK MARKETING}
Ili kuhakikisha
kwamba taasisi inasambaa katika nchi
mbalimbali duniani yaani wanapata Help
partners wengi kwa kadiri inavyowezekana na hivyo kuwafikia walengwa wengi zaidi (yaani wajane,yatima,
walio katika mazingira magumu) na kuhakikisha kwamba fedha ya kuwafadhili
walengwa inayotolewa kama kiingilio inaongezeka na hakuna ukwasi basi H2i ilibuni na kuamua kutumia mfumo wa biashara
ya mtandao ( Referal Marketing /Network marketing).
ü Biashara ya mtandao ni ya kupashana habari kati ya mtu na mtu, yaani unawashikisha fursa rafiki zako, jirani zako, waumini wenzio
nk. Hivyo basi baada ya wewe kujiunga utatakiwa kuwashirika watu wasiopungua wawili
wengine ambao nao pia watatakiwa watawatafute
watu wawili na kuendelea. Huzuiwi kuingiza idadi yoyote ya watu uliyonayo hata
kama ni watu 100! japo kiwango cha chini sana ni watu wawili.
(maelezo ya kina ya namna unavyoweza kupanda cheo toka cha 1hadi
cha 6 itafuata)
Huu ni mfumo
huu wa biashara ulionekana ni bora sana na rahisi kufanya. Asasi hii ilianza kuenea
na kupanuka na ikatoka nje na Asia na
mnamo mwaka Desemba 2013 H2i ilipoingia
Afrika kituo kikawa Lagos, Nigeria,
African Region Corporate Office
Jonathan Goodluck Estate
Cluster 26B, Flat 2
Isheri Olofin Alimosho LGA
Egbeda, Lagos, Nigeria
Kwa sasa
Helping Hands International inaenea kwa kasi katika nchi za Africa, tayari ipo
Benin,Ethiopia, Uganda,Kenya,Afrika Kusini,Ghana,Zambia,Msumbiji,Zimbabwe
na hatimaye Tanzania. Hapa kwetu Tanzania uzinduzi kitaifa umefanyika mwezi wa
saba Mwaka huu japo watu walianza kufanya kazi kabla ya uzinduzi.
Kwa ufafanuzi zaidi kuhusu Asasi hii / Kujiunga
Tembelea tovuti: www.helpinghandsinternational.biz
www.helpinghandsinternationaltanzania.blogspot.com
Call +255 622 673 000 Whatsapp +255 712 673 000 Email:
help2i.Tanzania@gmail.com

No comments:
Post a Comment